Genesis 2

1 aKwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo.

2 bKatika siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya, hivyo siku ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote. 3 cMungu akaibariki siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya.

Adamu Na Eva

4 dHaya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa.

Bwana Mungu alipoziumba mbingu na dunia,
5 ehapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa Bwana Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi, 6lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi: 7 fBwana Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi
Neno la Kiebrania la mavumbi ya ardhi ndilo kiini cha jina Adamu.
ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.

8 hBasi Bwana Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemuumba. 9 iBwana Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa kujua mema na mabaya.

10 jMto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni, kuanzia hapa ukagawanyika kuwa mito minne. 11 kMto wa kwanza uliitwa Pishoni, nao huzunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu. 12 l(Dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri, bedola na vito shohamu pia hupatikana huko.) 13Jina la mto wa pili ni Gihoni, ambao huzunguka nchi yote ya Kushi. 14 mJina la mto wa tatu ni Tigrisi, unaopita mashariki ya Ashuru. Mto wa nne ni Frati.

15 Bwana Mungu akamchukua huyo mtu, akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza. 16 nBwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wowote katika bustani, 17 olakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.”

18 p Bwana Mungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.”

19 qBasi Bwana Mungu alikuwa amefanyiza kutoka ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lolote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake. 20 rHivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani, na wanyama wote wa porini.

Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa.
21 sHivyo Bwana Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama. 22 tKisha Bwana Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.

23 uHuyo mwanaume akasema,

“Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu
na nyama ya nyama yangu,
ataitwa ‘mwanamke,’
Jina la Kiebrania la mwanamke linafanana na lile la mwanaume.

kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.”
24 wKwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

25 xAdamu na mkewe wote wawili walikuwa uchi, wala hawakuona aibu.

Copyright information for SwhNEN